ZEC_Kiswahili_1068.pdf

(97 KB) Pobierz
ZEKARIA
Utangulizi
Zekaria alianza huduma yake mnamo mwezi wa nane wa mwaka wa pili wa Dario (520 K.K.), miezi miwili
baada ya ujumbe wa kwanza wa Hagai. Maana ya jina Zekaria ni “BWANA amekumbuka.” Haijulikani kwa
uhakika Zekaria aliendelea kufanya huduma hiyo kwa muda gani.Kwa kadiri ionekanavyo alikuwa kijana (2:4)
wakati alipoanza huduma yake. Ido, ambaye ni babu yake (Zek 1:1) alikuwa miongoni mwa wale waliorudi kutoka
uhamishoni mwaka 538 K.K.
Katika ujumbe wake wa kwanza (1:1-6) Zekaria anawaonya watu ambao ndio kwanza tu walikuwa
wameanza kujenga upya hekalu kwamba inawapasa kusikiliza ujumbe wa Mungu kupitia manabii na kudumisha
uhusiano wa muhimu na Mungu, wasije wakaharakisha hukumu ya Mungu. Mfululizo wa maono ya usiku (1:7-
6:8) yanatia moyo wajenzi ule wakati mgumu katika hatua ya kukata tamaa.Ule utaratibu wa ujenzi ulikuwa
umesababisha maafisa wa Kiajemi kufanya uchunguzi na kuandika taarifa ya malalamiko kwa Dario (Ezr 5-6) .
Huenda Wayahudi walikuwa wakingojea hukumu ya Dario wakati Zekaria akitoa ujumbe wake uliowekewa msingi
katika haya maono ya usiku. Mtazamo wa jumla wa mfululizo wa maono haya manane yanawahakikishia wajenzi
kwamba Mungu anao mpango wa muda mrefu kwa ajili ya Israeli.
Miaka miwili baadaye, (518 K.K.) suala la kutia katika matendo kutii kufunga liliibuka (7:1-8:23). Zekaria kwa
mara nyingine anaangaliza watu kwamba njia ya kudumisha uhusiano sahihi na Mungu ni utii. Kule kufunga ili tu
kwamba mtu amefunga ni ubatili.Utaratibu wa kushika sheria kamwe hauwezi kutumika kama njia mbadala ya
kuonyesha upendo wa Mungu katika maisha ya kila siku. Sehemu ya mwisho ya ujumbe wa Zekaria (9-14)
haukuonyeshwa tarehe. Uwezekano mkubwa ni kwamba ulitolewa baadaye, huenda mnamo mwaka 480 K.K.
Hapa mkazo uko katika mpango wa maendeleo wa muda mrefu ukionyesha kusimamishwa kwa ufalme wa
mwisho. Mfalme anatambulishwa kama anayekuja kwa tabia ya unyenyekevu akileta wokovu lakini akikataliwa na
watu wake mwenyewe, yaani, Waisraeli, ambao baadaye wanaachwa kwenye hukumu ya mataifa. Mataifa
yatakapokusanyika kwa ajili ya vita dhidi ya Yerusalemu, Waisreli watamtambua Yeye “Yule waliomchoma mkuki”
(Zek.12:10) na wataibuka na ushindi. Ndipo mataifa yote yatakuja Yerusalemu kumwabudu Mfalme, Bwana wa
Majeshi.
Wazo Kuu
Zekaria anaonyesha kwamba Mungu ana mpango wa muda mrefu na Israeli, hivyo anaita mwito wa
utii.Anaonyesha jinsi ambavyo watu wanaweza kufanya mambo “ Si kwa nguvu wala kwa uwezo bali kwa Roho
Yangu ”asema.( 4:6).. Kuwapa watu wa Mungu matumaini kwa kuwajulisha watu mpango wa Mungu wa baadaye
wa ukombozi kupitia kwa Masiya.
.
Mambo Muhimu
Huu ujumbe wa mwanzoni unafuatiliwa na maono ambayo yaliwatia moyo wajenzi ambao Zekaria aliwatia
moyo kwa kuwaambia kwamba Mungu alikuwa na mpango mrefu kwa ajili ya Israeli.
Katika sura ya 7 na 8 Zekaria aliwataka watu wamtii Mungu, hii ikiwa ni njia ya kila mtu kumjali na kumhurumia
mwenzake. Mungu alitaka utii kwao katika kuhusiana naye.
Sura ya 9 mpaka 14 inazungumzia habari za miezi inayokuja, hukumu ya mwisho na kukua kwa muda mrefu
kwa ufalme wa mwisho.
Mwandishi
Zekaria
Mahali
Yerusalemu
Tarehe
520-470 K.K.
Wahusika
Hagai, Zerubabeli, Yoshua na waliorudi kutoka uhamishoni.
.
Mgawanyo
Wito wa kuwa watiifu . (1:1-6)
Maono. (1:7-6:15)
Hukumu dhidi ya maadui wa Israeli. (9:1-8)
1
ZEKARIA
Wito Wa Kumrudia BWANA
Katika mwezi wa nane wa mwaka wa pili
wa utawala wa mfalme Dario, neno la
BWANA lilimjia nabii Zekaria mwana wa
Berekia, mwana wa Iddo, kusema:
2 “BWANA aliwakasirikia sana baba zako wa
zamani. 3 Kwa hiyo waambie watu: Hivi ndivyo
BWANA Mwenye Nguvu asemavyo: ‘Nirudieni
mimi,’ asema BWANA Mwenye Nguvu, ‘Nami
nitawarudia ninyi,’ asema BWANA Mwenye
Nguvu. 4 Msiwe kama baba zenu, ambao
manabii waliotangulia waliwatangazia: Hivi
ndivyo BWANA Mwenye Nguvu asemavyo:
‘Geukeni, mziache njia zenu mbaya na matendo
yenu maovu.’ Lakini hawakunisikiliza wala
kufuata maelekezo yangu, asema BWANA.
5 Wako wapi baba zako sasa? Nao manabii, je,
wanaishi milele? 6 Je, maneno yangu na amri
zangu nilizowaagiza manabii watumishi wangu,
hayakuwapata baba zenu?’’
“Kisha walitubu na kusema, BWANA
Mwenye Nguvu ametutenda sawasawa na njia
zetu na matendo yetu yalivyostahili, kama
alivyokusudia kufanya.’ ’’
1
‘Nitairudia Yerusalemu kwa rehema na huko
nyumba yangu itajengwa tena. Nayo kamba ya
kupimia itanyooshwa Yerusalemu,’ asema
BWANA Mwenye Nguvu.
17 “Endelea kutangaza zaidi kwamba: Hivi
ndivyo asemavyo BWANA Mwenye Nguvu: ‘Miji
yangu itafurika tena usitawi na BWANA
atamfariji
Maono Ya Kwanza:
Mtu Katikati Ya Miti Ya Mihadasi
7 Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa
kumi na moja,yaani mwezi uitwao Shebati,
katika mwaka wa pili wa kutawala kwake mfalme
Dario, neno la BWANA lilimjia nabii Zekaria
mwana wa Berekia mwana wa Iddo.
8 Wakati wa usiku nilipata maono, mbele
yangu alikuwepo mtu akiendesha farasi
mwekundu! Alikuwa amesimama katikati ya miti
ya mihadasi kwenye bonde. Nyuma yake
walikuwepo farasi wekundu, wa kikahawia na
weupe.
9 Nikauliza, ‘‘Hivi ni vitu gani bwana wangu?’’
Malaika aliyekuwa akizungumza na mimi
akanijibu, ‘‘Nitakuonyesha kuwa ni nini.’’
10 Kisha yule mtu aliyesimama katikati ya miti
ya mihadasi akaeleza, ‘‘Ni wale ambao BWANA
amewatuma waende duniani kote.’’
11 Nao wakatoa taarifa kwa yule malaika wa
BWANA, aliyekuwa amesimama katikati ya miti
ya mihadasi, ‘‘Tumepita duniani kote na kukuta
ulimwengu wote umepumzika kwa amani.’’
12 Kisha malaika wa BWANA akasema,
‘‘BWANA Mwenye Nguvu, utazuia mpaka lini
rehema kutoka Yerusalemu na miji ya Yuda,
ambayo umeikasirikia kwa miaka hii sabini?’’
13 Kwa hiyo BWANA akazungumza maneno ya
upole na ya kufariji kwa malaika aliyezungumza
nami.
14 Kisha malaika yule aliyekuwa
akizungumza nami akasema, ‘‘Tangaza neno
hili: Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu asemalo:
‘Nina wivu sana kwa ajili ya Yerusalemu na
Sayuni, 15 lakini nimeyakasirikia sana mataifa
yanayojisikia kuwa yako salama. Nilikuwa
nimewakasirikia Israeli kidogo tu, lakini mataifa
hayo yaliwazidishia maafa.’
tena
Sayuni
na
kumchagua
Yerusalemu.’ ’’
Maono Ya Pili:
Pembe Nne Na Mafundi Wanne
18 Kisha nikatazama juu, na pale mbele
yangu nikaona pembe nne! 19 Nikamwuliza yule
malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Ni nini
hivi?’’
Akanijibu, “Hizi ni zile pembe
zilizowatawanya Yuda, Israeli na Yerusalemu.’’
20 Kisha BWANA akanionyesha mafundi
wanne.
21 Nikauliza, “Hawa wanakuja kufanya
nini?’’
Akanijibu, “Hizi ndizo pembe
zilizowatawanya Yuda ili asiwepo atakayeweza
kuinua kichwa chake, lakini mafundi wamekuja
kuzitia hofu na kuzitupa chini hizi pembe za
mataifa ambayo yaliinua pembe zao dhidi ya
nchi ya Yuda na kuwatawanya watu wake.’’
Maono Ya Tatu:
Mtu
Mwenye Kamba Ya Kupimia
2
Kisha nikatazama juu, pale mbele yangu
alikuwepo mtu mwenye kamba ya kupimia
mkononi mwake! 2 Nikamwuliza, “Unakwenda
wapi?’’
Akanijibu, “Kupima Yerusalemu, kupata
urefu na upana wake.’’
3 Kisha malaika aliyekuwa akizungumza
nami akaondoka, malaika mwingine akaja
kukutana naye 4 na kumwambia: “Kimbia,
umwambie yule kijana, ‘Yerusalemu utakuwa mji
usio na kuta kwa sababu ya wingi wa watu na
16 ‘‘Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyo BWANA:
2
952110278.003.png
 
ZEKARIA
mifugo iliyomo. 5 Mimi mwenyewe nitakuwa
ukuta wa moto kuuzunguka,’ asema BWANA,
‘nami nitakuwa utukufu wake ndani yake.’
6 “Njoni! Njoni! Kimbieni mtoke katika nchi ya
kaskazini,’’ asema BWANA, “Kwa kuwa
nimewatawanya kwenye pande nne za mbingu,’’
asema BWANA.
7 “Njoo, Ee Sayuni! Kimbia, wewe uishiye
ndani ya Binti Babeli!’’ 8 Kwa kuwa hivi ndivyo
asemavyo BWANA Mwenye Nguvu: “Baada ya
yeye kuniheshimu na kunituma mimi dhidi ya
mataifa yaliyokuteka wewe nyara, kwa kuwa ye
yote awagusaye ninyi, anaigusa mboni ya jicho
lake, 9 hakika nitauinua mkono wangu dhidi yao
ili watumwa wao wawateke nyara. Ndipo
mtakapojua ya kwamba BWANA Mwenye
Nguvu amenituma.
10 “Piga kelele na ufurahie, Ee Binti Sayuni,
kwa maana ninakuja, nami nitaishi miongoni
mwenu,’’ asema BWANA. 11 “Mataifa mengi
yataunganishwa na BWANA siku hiyo, nao
watakuwa watu wangu. Nitaishi miongoni
mwenu nanyi mtajua kwamba BWANA Mwenye
Nguvu amenituma kwenu. 12 BWANA atairithi
Yuda kama fungu lake katika nchi takatifu na
atachagua tena Yerusalemu. 13 Tulieni mbele za
BWANA, enyi watu wote, kwa sababu ameinuka
kutoka makao yake matakatifu.”
6 Malaika wa BWANA akamwamuru Yoshua:
7 “Hivi ndivyo asemavyo BWANA Mwenye
Nguvu: ‘Ikiwa utakwenda katika njia zangu na
kushika masharti yangu, basi utaitawala nyumba
yangu na kuwa na amri juu ya nyua zangu, nami
nitakupa
nafasi
miongoni
mwa
hawa
wasimamao hapa.
8 ‘‘ ‘Sikiliza, Ee Yoshua kuhani mkuu, pamoja
na wenzako walioketi mbele yako, ambao ni
watu ishara ya mambo yatakayokuja:
Ninakwenda kumleta mtumishi wangu, Tawi.
9 Tazama, jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua!
Kuna macho saba juu ya jiwe lile moja, nami
nitachora maandishi juu yake,’ asema BWANA
Mwenye Nguvu, ‘nami nitaiondoa dhambi ya
nchi hii kwa siku moja.
10 “ ‘Katika siku hiyo kila mmoja wenu
atamwalika jirani yake akae chini ya mzabibu
wake na mtini wake,’ asema BWANA Mwenye
Nguvu.’
Maono Ya Tano:
Kinara Cha Taa Cha Dhahabu Na Mizeituni
Miwili
4
Kisha malaika aliyezungumza nami
akarudi na kuniamsha, kama mtu
aamshwavyo kutoka katika usingizi wake.
2 Akaniuliza, “Unaona nini?’’
Nikajibu, “Ninaona kinara cha taa cha
dhahabu tupu, nacho kina bakuli juu yake na taa
zake saba juu yake, tena iko mirija saba ya
kuleta mafuta, kwenye taa zote zilizo juu yake.
3 Pia kuna mizeituni miwili karibu yake, mmoja
upande wa kuume wa bakuli na mwingine
upande wa kushoto.’’
4 Nikamuuliza malaika aliyezungumza nami,
“Hivi ni vitu gani, bwana wangu?’’
5 Akanijibu, “Hujui kuwa hivi ni vitu gani?’’
Nikajibu, “Hapana, bwana wangu.’’
6 Kisha akaniambia, “Hili ni neno la BWANA
kwa Zerubabeli: ‘Si kwa nguvu, wala si kwa
uwezo, bali ni kwa Roho yangu,’ asema BWANA
Mwenye Nguvu.
7 ‘‘Wewe ni kitu gani, Ee mlima mkubwa
sana? Mbele ya Zerubabeli wewe utakuwa ardhi
tambarare. Kisha ataweka jiwe la juu kabisa la
mwisho na watu wakipiga kelele wakisema,
‘Mungu libariki! Mungu libariki!’’
8 Kisha neno la BWANA likanijia: 9 ‘‘Mikono
ya Zerubabeli iliweka msingi wa hekalu hili,
mikono yake pia italimalizia. Kisha mtajua ya
kuwa BWANA Mwenye Nguvu amenituma mimi
kwenu.
Maono Ya Nne:
Mavazi Safi Kwa Ajili Ya Kuhani Mkuu
Kisha akanionyesha Yoshua kuhani mkuu
akiwa amesimama mbele ya malaika wa
BWANA, naye Shetani amesimama upande
wake wa kuume ili amshitaki. 2 BWANA
akamwambia Shetani, “BWANA akukemee
Shetani! BWANA, ambaye ameichagua
Yerusalemu, akukemee! Je, mtu huyu siyo
kijinga kinachowaka kilichonyakuliwa kwenye
moto?’’
3 Wakati huu, Yoshua alikuwa amevaa nguo
chafu alipokuwa amesimama mbele ya malaika.
4 Malaika akawaambia wale waliokuwa
wamesimama mbele yake, ‘‘Mvueni nguo zake
chafu.’’
Kisha akamwambia Yoshua, ‘‘Tazama,
nimeiondoa dhambi yako, nami nitakuvika
mavazi ya kitajiri.’’
5 Kisha nikasema, “Mvike kilemba kilicho safi
kichwani mwake.’’ Kwa hiyo wakamvika kilemba
safi kichwani na kumvika yale mavazi mengine,
wakati malaika wa BWANA akiwa amesimama
karibu.
3
3
952110278.004.png
 
ZEKARIA
10 ‘‘Ni nani anayeidharau siku ya mambo
madogo? Watu watashangilia watakapoona
timazi mkononi mwa Zerubabeli.
“(Hizi saba ni macho ya BWANA ambayo
huzunguka duniani kote.)’’
11 Kisha nikamwuliza yule malaika, “Hii
mizeituni miwili iliyoko upande wa kuume na wa
kushoto wa kinara cha taa ni nini?”
12 Tena nikamwuliza, “Haya matawi mawili
ya mizeituni karibu na hiyo mirija miwili ya
dhahabu inayomimina mafuta ya dhahabu ni
nini?’’
13 Akajibu, “Hujui kuwa haya ni nini?’’
Nikamjibu, “Hapana, bwana wangu.’’
14 Kwa hiyo akasema, “Hawa ni wawili
ambao wamepakwa mafuta ili kumtumikia
Bwana wa dunia yote.’’
9 Kisha nikatazama juu na mbele yangu,
walikuwepo wanawake wawili, wakiwa na upepo
katika mabawa yao! Walikuwa na mabawa kama
ya korongo, nao wakainua kile kikapu na kuruka
nacho kati ya mbingu na nchi.
10 Nikamwuliza yule malaika aliyekuwa
akizungumza nami, ‘‘Wanakipeleka wapi hicho
kikapu?’’
11 Akanijibu, ‘‘Wanakipeleka katika nchi ya
Babeli na kujenga nyumba kwa ajili yake.
Itakapokuwa tayari, kikapu kitawekwa pale
mahali pake.’’
Maono Ya Nane: Magari Manne Ya Vita
Nikatazama juu tena, nikaona mbele yangu
magari manne ya vita yakija kutoka kati ya
milima miwili, milima ya shaba! 2 Gari la kwanza
lilivutwa na farasi wekundu, la pili lilivutwa na
farasi weusi, 3 la tatu lilivutwa na farasi weupe na
gari la nne lilivutwa na farasi wa madoadoa ya
kijivu, wote wenye nguvu. 4 Nikamwuliza malaika
aliyekuwa akizungumza nami, ‘‘Hawa ni nani
bwana wangu?’’
5 Malaika akanijibu, ‘‘Hizi ni roho nne za
mbinguni zisimamazo mbele ya uwepo wa
Bwana wa dunia yote, zinatoka kwenda kufanya
kazi yake. 6 Gari linalovutwa na farasi weusi
linaelekea katika nchi ya kaskazini, la farasi
weupe linaelekea magharibi na la farasi wa
madoadoa ya kijivu linaelekea kusini.’’
7 Wakati hao farasi wenye nguvu walipokuwa
wakitoka, walikuwa wakijitahidi kwenda duniani
kote. Akasema, ‘‘Nenda duniani kote!’’ kwa hiyo
wakaenda duniani kote.
8 Kisha akaniita, “Tazama, wale
wanaokwenda kuelekea nchi ya kaskazini
wamepumzisha Roho yangu katika nchi ya
kaskazini.’’
6
Maono Ya Sita: Gombo Linaloruka
Nikatazama tena, mbele yangu kulikuwa
na kitabu kilichoruka!
2 Akaniuliza, “Unaona nini?’’
Nikamjibu, “Naona kitabu kinachoruka
chenye,urefu wa dhiraa ishirini a na upana wa
dhiraa kumi b .’’
3 Akaniambia, “Hii ni laana inayotoka kwenda
juu ya nchi yote, kwa kuwa kufuatana na yale
yaliyoandikwa katika upande mmoja, kila mwizi
atahamishwa, pia kufuatana na yaliyo upande
wa pili, kila aapaye kwa uongo atahamishwa.
4 BWANA Mwenye Nguvu asema, ‘Nitaituma
hiyo laana, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi
na nyumba ya huyo aapaye kwa uongo kwa jina
langu. Itabaki katika nyumba yake na kuiharibu,
pamoja na mbao zake na mawe yake.’ ’’
5
Maono Ya Saba: Mwanamke Ndani Ya Kikapu
5 Kisha yule malaika aliyekuwa akizungumza
nami akanijia na kuniambia, “Tazama juu uone
ni nini kile kinachojitokeza.’’
6 Nikamwuliza, “Ni kitu gani?’’ Akanijibu, ‘‘Ni
kikapu cha kupimia.’’ Kisha akaongeza kusema,
‘‘Huu ni uovu wa watu katika nchi nzima.’’
7 Kisha kifuniko kilichotengenezwa kwa
madini ya risasi kilichokuwa kimefunika kile
kikapu, kiliinuliwa na ndani ya kile kikapu
alikuweko mwanamke ameketi! 8 Akasema, ‘‘Huu
ni uovu,’’ akamsukumia ndani ya kikapu na
kushindilia kifuniko juu ya mdomo wa kikapu.
Taji Kwa Ajili Ya Yoshua.
9 Neno la BWANA likanijia kusema:
10 ‘‘Chukua fedha na dhahabu kutoka kwa watu
waliohamishwa yaani Heldai, Tobia na Yedaya
ambao wamefika kutoka Babeli. Siku iyo hiyo
nenda nyumbani kwa Yosia mwana wa Sefania.
11 Chukua fedha na dhahabu utengeneze taji,
nawe uiweke kichwani mwa kuhani mkuu
Yoshua, mwana wa Yehosadiki. 12 Umwambie,
hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu:
‘Huyu ndiye mtu ambaye jina lake ni Tawi, naye
atachipua kutoka mahali pake na kujenga
hekalu la BWANA. 13 Ni yeye atakayejenga
hekalu la BWANA, naye atavikwa utukufu na
a 2 ‘‘dhiraa ishirini’’ ni sawa na mita 9.
b 2 ‘‘dhiraa kumi’’ ni sawa na mita 4.5
4
952110278.001.png
 
ZEKARIA
ataketi kumiliki katika kiti cha enzi naye atakuwa
kuhani katika kiti chake cha enzi. Hapo
patakuwa amani kati ya hao wawili.’ 14 Taji
itatolewa kwa Heldai, Tobia, Yedaya na Heni
mwana wa Sefania kama kumbukumbu ndani ya
hekalu la BWANA. 15 Wale walio mbali sana
watakuja na kusaidia kulijenga hekalu la
BWANA, nanyi mtajua ya kwamba BWANA
Mwenye Nguvu amenituma kwenu. Hili litatokea
ikiwa mtamtii BWANA, Mungu wenu kwa bidii.’’
walikuwa wageni. Nchi ikaachwa ukiwa nyuma
yao kiasi kwamba hakuna aliyeweza kuingia au
kutoka. Hivi ndivyo walivyoifanya ile nchi
iliyokuwa imependeza kuwa ukiwa.’ ’’
BWANA Anaahidi Kuibariki
Yerusalemu
Neno la BWANA Mwenye Nguvu likanijia
tena. 2 Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye
Nguvu: “Nina wivu sana kwa ajili ya Sayuni,
ninawaka wivu kwa ajili yake.”
3 Hiii ndilo asemalo BWANA: “Nitarudi
Sayuni na kufanya makao Yerusalemu. Kisha
Yerusalemu utaitwa mji wa kweli, mlima wa
BWANA Mwenye Nguvu utaitwa Mlima
Mtakatifu.’’
4 Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu:
“Kwa mara nyingine tena wazee wanaume kwa
wanawake walioshiba umri wataketi katika
barabara za Yerusalemu, kila mmoja akiwa na
mkongojo wake mkononi kwa sababu ya umri
wake. 5 Barabara za mji zitajaa wavulana na
wasichana wanaocheza humo.’’
6 Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu:
“Mambo haya yanaweza kuonekana ya ajabu
kwa mabaki ya watu wakati huo, lakini yaweza
kuwa ya ajabu kwangu?’’ asema BWANA
Mwenye Nguvu.
7 Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu:
“Nitawaokoa watu wangu kutoka nchi za
mashariki na magharibi. 8 Nitawarudisha waje
kuishi Yerusalemu, watakuwa watu wangu nami
nitakuwa mwaminifu na wa haki kwao kama
Mungu wao.’’
9 Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu:
“Ninyi ambao sasa mnasikia maneno haya
yanayozungumzwa na manabii ambao
walikuwepo wakati wa kuwekwa kwa msingi wa
nyumba ya BWANA Mwenye Nguvu, mikono
yenu na iwe na nguvu ili hekalu liweze
kujengwa. 10 Kabla ya wakati huo, hapakuwepo
na ujira kwa mtu wala mnyama. Hakuna mtu
aliyeweza kufanya shughuli yake kwa usalama
kwa sababu ya adui yake, kwa kuwa nilikuwa
nimemfanya kila mtu adui wa jirani yake.
11 Lakini sasa sitawatendea mabaki ya watu
hawa kama nilivyowatenda zamani,’’ asema
BWANA Mwenye Nguvu.
12 “Mbegu itakua vizuri, mzabibu utazaa
matunda yake, ardhi itatoa mazao yake, na
mbingu zitadondosha umande wake. Vitu hivi
vyote nitawapa mabaki ya watu kama urithi wao.
13 Jinsi mlivyokuwa kitu cha laana katikati ya
8
Hak
i Na Rehema, Sio Kufunga
Katika mwaka wa nne wa utawala wa
mfalme Dario, neno la BWANA lilimjia
Zekaria siku ya nne ya mwezi wa tisa, mwezi wa
Kisleu. 2 Watu wa Betheli walikuwa wamemtuma
Shareza na Regam-meleki pamoja na watu wao,
kumsihi BWANA 3 kwa kuwauliza makuhani wa
nyumba ya BWANA Mwenye Nguvu na manabii,
“Je, imempasa kuomboleza na kufunga katika
mwezi wa tano, kama ambavyo nimekuwa
nikifanya kwa miaka mingi?”
7
4 Kisha neno la BWANA Mwenye Nguvu
likanijia kusema: 5 “Waulize watu wote wa nchi
na makuhani, ‘Je, mlipofunga na kuomboleza
katika mwezi wa tano na wa saba kwa miaka
sabini iliyopita, mlifunga kweli kwa ajili yangu?
6 Na mlipokuwa mkila na kunywa, je, hamkuwa
mnasheherekea kwa ajili ya nafsi zenu? 7 Je,
haya sio maneno ya BWANA aliyosema kupitia
manabii waliotangulia, wakati Yerusalemu
pamoja na miji inayoizunguka ilipokuwa katika
hali ya utulivu na ya mafanikio, wakati Negebu
na Shefala zikiwa zimekaliwa na watu?’ ’’
8 Neno la BWANA likamjia tena Zekaria:
9 “Hivi ndivyo asemavyo BWANA Mwenye
Nguvu: ‘Fanyeni hukumu za haki, onyesheni
rehema na huruma ninyi kwa ninyi.
10 Msimwonee mjane wala yatima, mgeni wala
maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu
ninyi kwa ninyi.’
11 “Lakini wakakataa kusikiliza, wakanipa
kisogo kwa ukaidi na kuziba masikio yao.
12 Wakaifanya mioyo yao migumu kama jiwe
gumu na hawakuisikiliza sheria au maneno
ambayo BWANA Mwenye Nguvu aliyatuma kwa
njia ya Roho wake kupitia manabii waliotangulia.
Kwa hiyo BWANA Mwenye Nguvu alikasirika
sana.
13 ‘Wakati nilipoita, hawakusikiliza, kwa hiyo
walipoita, sikusikiliza,’ asema BWANA Mwenye
Nguvu. 14 ‘Niliwatawanya kwa upepo wa kisulisuli
miongoni mwa mataifa yote, mahali ambapo
5
952110278.002.png
 
Zgłoś jeśli naruszono regulamin