2PE_Kiswahili_1068.pdf

(38 KB) Pobierz
2Petro
Utangulizi
Barua hii iliandikwa muda mfupi tu kabla ya kifo cha Petro na inagusia matatizo ambayo aliona yangebaki
baada ya kifo chake. Anawahimiza waamini waendelee kukua kiroho wakiitambua kweli iliyomo katika Injili ya
Kristo. Kweli hii haitokani na hadithi za kale bali inatokana na mambo yaliyoonekana kwa macho. Anawaonya
kuhusu walimu wa uongo ambao wangetukuza mawazo yao wenyewe badala ya mafundisho ya kweli ya Neno la
Mungu. Hatimaye anakumbusha kwamba Kristo atakuja siku moja kuangamiza hali ya asili ya ulimwengu huu na
kwa sababu hii hatuna sababu ya kuung'ang'ania sana.
Wazo Kuu
Waraka wa Pili wa Petro unakaza juu ya umuhimu wa kusimama imara wakati ambapo kuna mafundisho
mengi ya kupotosha. Kiini kikuu cha waraka huu ni “maarifa”, yaani, kupata ujuzi na “kujua”, neno ambalo
limetajwa mara kumi na sita. Hatari inayowakabili hawa wasomaji sasa haikuwa mateso kama ilivyokuwa wakati
waraka wa kwanza ulipoandikwa, bali upotovu kuhusu tumaini la mambo ya mwisho, uliokuwa ukitangazwa na
walimu wa uongo na watenda maovu waliokuwa wamejiingiza ndani ya kanisa. Watu wa dunia wanajitahidi
kuiharibu kazi ya Mungu lakini sisi tunaoamini hatuna budi kuepuka majaribu yote, tuishi maisha ya kumcha
Mungu, tuamini la kweli, tuvumilie mateso, tumwamini Mungu na kungojea kurudi Kwake Kristo.
Mwandishi
Yale maneno ya ufunguzi yenyewe yanamtambulisha kuwa mwandishi wa waraka huu ni “Simoni Petro,
mtumishi na mtume wa Yesu Kristo.” Maadam kuna ushahidi kutoka nje ya kanisa la kwanza kuuhesabia waraka
huu kuwa umeandikwa na Mtume Petro, wasomi wengine wametia shaka uhalisi wa uandishi kuwa wa Petro kwa
msingi kwamba ile tofauti ya mtindo wa uandishi wa nyaraka hizi mbili, kutajwa kwa Paulo (3:15–16) na ule
mfafanuo kati ya 2Petro na Yuda.
Lakini, hata hivyo, kuna ushahidi wa ndani unaoashiria kuwa Petro ndiye mwandishi. Kule kutambulisha
mwandishi kama “Simoni Petro” kunaelekea kuwa halisi kwa kuwa kama angekuwa ni mtu anyejifanya angetumia
“Petro” ili aweze kufuata mtriririko wa waraka wa kwanza.Ule uandishi wa kibinafsi na msamiati unalinganishwa
na maisha na mahubiri ya Petro.Ile jinsi ya kusema na yale mawazo yaliyomo vina mfanano mkubwa kati ya hizi
nyaraka mbili zinazohesabiwa kuwa za Petro.
Tarehe
Waraka huu uliandikwa kati ya 65 na 68 B.K., muda mfupi tu kabla ya kifo cha Petro, nao unaandikiwa wasomaji
wale wale ambao Petro alikuwa akiwatia moyo katika waraka wa kwanza.
Mahali
Uwezekano mkubwa ni kwamba waraka huu mwandishi alikuwa Rumi wakati wa kuuandika.
Mgawanyo
Namna ya kukua kiroho (1:1-21)
Maonyo kuhusu walimu wa uongo (2:1-22)
Maagizo juu ya kuja kwake Kristo mara ya pili (3:1-18).
1
2Petro
mambo haya sikuzote.
16 Tulipowafundisha juu ya uweza na kuja
kwa Bwana wetu Yesu Kristo, hatukufuata
hadithi zilizotungwa kwa werevu, bali
tulishuhudia kwa macho yetu utukufu wake.
17 Maana alipewa heshima na utukufu kutoka
kwa Mungu Baba sauti ilipomjia katika Utukufu
Mkuu ikisema, ‘‘Huyu ni Mwanangu, mpendwa
Wangu, ninayependezwa naye'',
18 Sisi wenyewe tuliisikia sauti hii ambayo ilitoka
mbinguni, wakati tulipokuwa pamoja Naye
kwenye ule mlima mtakatifu.
19 Nasi tunalo pia neno la hakika zaidi la
unabii, ambalo mtafanya vema mkiliangalia kwa
bidii, kama vile nuru inayong’aa gizani, hadi
kupambazuka na nyota ya asubuhi itokee
mioyoni mwenu. 20 Awali ya yote, yawapasa
mjue kwamba hakuna unabii katika Maandiko
uliofasiriwa kama apendavyo mtu mwenyewe.
21 Kwa maana unabii haukuja kamwe kwa
mapenzi ya mwanadamu, bali watu walinena
yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho
Mtakatifu.
Salamu
Simoni Petro mtumishi na mtume wa
Yesu Kristo,
1
Kwa wale ambao kwa njia ya haki ya Mungu
wetu na Yesu Kristo mmepokea imani iliyo na
thamani kama yetu:
2 neema na amani iwe kwenu kwa wingi
katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu.
Wito Wa Mkristo Na Uteule
3 Uweza Wake wa uungu umetupatia
mambo yote tunayohitaji kwa ajili ya uzima na
uchaji wa Mungu, kwa kumjua Yeye aliyetuita
kwa utukufu Wake na wema Wake mwenyewe.
4 Kwa sababu hiyo, ametukirimia ahadi Zake kuu
na za thamani kupitia mambo haya, ili kwa
kupitia hayo mpate kuokoka na upotovu ulioko
duniani kwa sababu ya tamaa mbaya.
5 Kwa sababu hii, jitahidini sana katika imani
yenu kuongeza wema na katika wema wenu
maarifa, 6 katika maarifa yenu kiasi; katika kiasi,
saburi, katika saburi yenu, utauwa, 7 katika
utauwa wenu upendano wa kidugu, katika
upendano wa kidugu, upendo. 8 Kwa maana
haya yakiwa kwenu kwa wingi, nayo yakizidi
kuongezeka yanawafanya kuwa wenye bidii na
wenye kuzaa matunda katika kumjua Bwana
wetu Yesu Kristo. 9 Kwa kuwa mtu asiyekuwa na
mambo haya haoni mbali, pia ni kipofu, naye
amesahau kule kutakaswa kwa dhambi zake za
zamani.
10 Kwa hiyo, ndugu zangu, fanyeni bidii zaidi
kuuthibitisha wito wenu na uteule wenu, kwa
maana mkifanya hivyo, hamtajikwaa kamwe.
11 Kwa njia hii, mtajaliwa kwa ukarimu mwingi
kuingia katika Ufalme wa milele wa Bwana na
Mwokozi wetu Yesu Kristo.
Manabii Wa Uongo Na Adhabu Yao
Lakini pia waliinuka manabii wa uongo
miongoni mwa watu, kama vile
watakavyokuwako walimu wa uongo miongoni
mwenu, ambao kwa siri, wataingiza mafundisho
yasiyopatana na kweli hata kumkana Bwana wa
pekee aliyewanunua na kujiletea juu yao
maangamizi ya haraka. 2 Hata hivyo, wengi
watafuata njia zao za ufisadi ambao kwa ajili
yao njia ya kweli itatukanwa. 3 Nao katika tamaa
yao watajipatia faida kwenu kwa maneno ya
madanganyo waliyotunga wenyewe. Lakini
hukumu imekwisha kutangazwa dhidi yao tangu
zamani, ambayo haikawii wala ungamivu wao
haujalala usingizi.
4 Kwa maana kama Mungu hakuwasamehe
malaika walipotenda dhambi, bali aliwatupa
kuzim u a , katika vifungo vya giza wakae humo
mpaka ije hukumu, 5 kama hakuusamehe
ulimwengu wa kale alipoleta gharika juu ya watu
wale wasiomcha Mungu, akamhifadhi Noa,
mhubiri wa haki, pamoja na watu wengine saba,
6 kama aliihukumu miji ya Sodoma na Gomora
kwa kuiteketeza kwa moto ikawa majivu na
kuifanya kuwa kielelezo kwa wote ambao
2
Unabii Wa Maandiko
12 Hivyo nitawakumbusha mambo haya
sikuzote, hata ingawa mnayajua na
yamethibitishwa katika kweli mliyo nayo.
13 Naona ni vema kuwaamsha kwa
kuwakumbusha mambo haya wakati wote
niwapo katika hema hili ambalo ni mwili wangu.
14 Kwa sababu najua ya kwamba karibuni
nitaliweka kando, kama vile Bwana wetu Yesu
Kristo alivyoliweka wazi kwangu. 15 Nami
nitafanya kila juhudi kuona kwamba baada ya
kuondoka kwangu mtaweza kuyakumbuka
a 4 “Kuzimu” linatokana na neno la Kiyunani “Tartarus” ambalo
maana yake “chini sana, mahali pa mateso kwa watu
waliopotea”
2
952118052.002.png
 
2Petro
hawatamcha Mungu 7 na kama alimwokoa Loti,
mtu mwenye haki, ambaye alihuzunishwa na
maisha machafu ya watu wapotovu 8 (kwa
sababu yale matendo mapotovu aliyoyaona na
kuyasikia huyo mtu mwenye haki alipoishi
miongoni mwao yalimhuzunisha siku baada ya
siku), 9 ikiwa hivyo ndivyo, basi Bwana anajua
jinsi ya kuwaokoa wacha Mungu kutoka katika
majaribu na kuwaweka waasi katika adhabu
hadi siku ya hukumu. 10 Hii ni hakika hasa kwa
wale wanaofuata tamaa mbaya za mwili na
kudharau mamlaka.
Kwa ushupavu na kwa kiburi watu hawa
hawaogopi kunena mabaya dhidi ya viumbe vya
mbinguni, 11 lakini hata malaika, ingawa wana
nguvu na uwezo zaidi, hawaleti mashtaka dhidi
ya viumbe kama hao mbele za Bwana. 12 Lakini
watu hawa hukufuru katika mambo
wasiyoyafahamu. Wao ni kama wanyama wasio
na akili, viumbe wanaotawaliwa na hisia za
mwili, waliozaliwa ili wakamatwe na kuchinjwa.
Wao husingizia wasiyoyafahamu na wanyama
hao
wakanaswa tena na kushindwa, hali yao ya
mwisho ni mbaya zaidi kuliko ile ya kwanza.
21 Ingelikuwa afadhali kwao kama wasingeliijua
kamwe njia ya haki, kuliko kuijua kisha
wakaiacha ile amri takatifu waliyokabidhiwa.
22 Imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya
kweli isemayo, “Mbwa ameyarudia matapishi
yake mwenyewe,’’ tena nyingine yasema,
“Nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa
matopeni.’’
Ahadi Ya Kuja Kwa Bwana
Wapenzi, huu ndio waraka wa pili
ninaowaandikia. Katika nyaraka hizi mbili
ninajaribu kuziamsha nia zenu safi kwa
kuwakumbusha kwamba, 2 nataka ninyi
mkumbuke maneno yaliyosemwa zamani na
manabii watakatifu na ile amri ya Bwana na
Mwokozi mliyopewa kwa kupitia kwa mitume
wenu.
3 Kwanza kabisa ni lazima mfahamu ya
kwamba siku za mwisho watakuja watu wenye
dhihaka wakidhihaki na kuzifuata tamaa zao
mbaya. 4 na kusema, “Iko wapi ile ahadi ya kuja
Kwake? Tangu baba zetu walipokufa, kila kitu
kinaendelea kama kilivyokuwa tangu mwanzo
wa kuumbwa.’’ 5 Wao kwa makusudi hupuza
ukweli huu, ya kwamba kwa neno la Mungu
mbingu zilikuwepo tangu zamani nayo dunia
ilifanyizwa kutoka ndani ya maji na kwa hayo
maji, 6 ulimwengu wa wakati ule uligharikishwa
na kuangamia. 7 Lakini kwa neno lilo hilo mbingu
za sasa na dunia, zimewekwa akiba kwa ajili ya
moto, zikihifadhiwa hadi siku ile ya hukumu na
ya kuangamizwa kwa watu wasiomcha Mungu.
8 Lakini wapenzi, msisahau neno hili,
kwamba kwa Bwana, siku moja ni kama miaka
elfu na miaka elfu ni kama siku moja. 9 Bwana
hakawii kuitimiza ahadi Yake kama watu
wengine wanavyodhani kukawia, bali Yeye
anawavumilia, maana hataki mtu ye yote
aangamie, bali kila mmoja afikilie toba.
10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi.
Ndipo mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu na
vitu vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo
dunia na kila kitu kilichomo ndani yake
kitaunguzwa.
11 Kwa kuwa vitu vyote vitayeyuka hivyo,
ninyi je, imewapasa kuwa watu wa namna gani?
Inawapasa kuishi maisha matakatifu na ya
kumcha Mungu, 12 mkingojea na kuhimiza kuja
kwa hiyo siku ya Mungu, ambayo siku hiyo
mbingu zitachomwa moto na kutoweka na vitu
3
watakapoangamizwa,
hawa
nao
wataangamizwa pia.
13 Watalipwa madhara kwa ajili ya madhara
waliyowatendea wengine. Huhesabu kuwa ni
anasa kufanya karamu za ulevi na ulafi wakati
wa mchana. Wao ni mawaa na dosari katika
karamu zenu wakijifurahisha kwa ulevi na ulafi
katika anasa zao wanaposhiriki katika karamu
zenu. 14 Wakiwa na macho yaliyojaa uzinzi,
hawaachi kutenda dhambi. Huwashawishi wale
wasio imara, wao ni hodari kwa kutamani, wana
wa laana! 15 Wameiacha njia iliyonyoka,
wakapotoka na kuifuata njia ya Balaamu mwana
wa Beori aliyependa mshahara wa uovu.
16 Lakini Balaamu kwa ajili ya uovu wake,
alikemewa na punda, mnyama asiyejua
kusema, akaongea akitumia sauti ya
mwanadamu na kuzuia wazimu wa huyo nabii.
17 Watu hawa ni chemchemi zisizo na maji
na ukungu upeperushwao na tufani, ambao giza
nene limewekwa tayari kwa ajili yao. 18 Kwa
maana wao hunena maneno makuu mno ya
upumbavu na kwa tamaa mbaya za uasherati
huwashawishi watu ambao ndipo tu
wamejiondoa miongoni mwa wale wanaoishi
katika ufisadi. 19 Huwaahidi uhuru hao
waliowanasa, wakati wao wenyewe ni watumwa
wa ufisadi. Kwa maana mtu ni mtumwa wa kitu
cho chote kinachomtawala. 20 Kwa kuwa kama
wameukimbia upotovu wa dunia kwa kumjua
Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo, kisha
3
952118052.003.png
 
2Petro
vya asili vitayeyuka kwa moto. 13 Lakini
kufuatana na ahadi Yake, sisi tunatazamia kwa
furaha mbingu mpya na dunia mpya, ambayo
haki hukaa ndani yake.
14 Kwa sababu hii, wapenzi, kwa kuwa
mnatazamia kwa furaha mambo haya, fanyeni
bidii ili awakute katika amani, bila mawaa wala
dosari. 15 Nanyi hesabuni uvumilivu wa Bwana
kuwa ni wokovu, kama vile ndugu yetu mpenzi
Paulo alivyowaandikia kwa hekima ile aliyopewa
na Mungu. 16 Huandika vivyo hivyo katika
nyaraka zake zote akizungumzia ndani yake
mambo haya. Katika nyaraka zake kuna mambo
mengine ambayo ni vigumu kuyaelewa, ambayo
watu wajinga na wasio thabiti huyapotosha kwa
maangamizi yao wenyewe, kama wapotoshavyo
pia Maandiko mengine.
17 Basi, ninyi wapenzi, kwa kuwa
mmekwisha kujua mambo haya, jilindeni msije
mkachukuliwa na kosa la watu hao waasi na
kuanguka kutoka kwenye uthabiti wenu. 18 Bali
kueni katika neema na katika kumjua Bwana na
Mwokozi wetu Yesu Kristo. Utukufu una Yeye
sasa na milele! Amen.
4
952118052.001.png
 
Zgłoś jeśli naruszono regulamin