2CO_Kiswahili_1068.pdf

(80 KB) Pobierz
2Wakorinto
Utangulizi
Ingawa inaonekana kwamba waraka wa kwanza wa Paulo kwa Wakorintho uliwasaidia wakristo wa Korintho,
lakini bado kulikuwa na mambo mengine ya kurekebisha kwani haukumaliza matatizo yote. Bado kulikuwa na
mivutano na mashindano yaliyokuwa yakiendelea ndani ya kanisa la Korintho. Walimu wa uongo walikuwa
wamejiingiza ndani ya kanisa wakiwa wanapinga na hata kushambulia uadilifu wa Paulo mwenyewe na mamlaka
yake kama mtume.Wengine katika kanisa hawakutaka kutubu. Hivyo Paulo akisukumwa na upendo na kuhusika
kwake, aliamua kutokurudi huko hadi tabia zao zibadilike.
Paulo akiwa na wasiwasi na kanisa la Korintho, alitoka Efeso akaenda Troa, ambapo alivunjika moyo kwa
kutokupata habari zo zote kutoka Korintho (2:12 – 13). Paulo alipofika Makedonia aliburudishwa na Timotheo
alipomletea habari nzuri kwamba uamsho ulikuwa umeanza katika kanisa la Korintho.
Huu ndio wakati Paulo alipoandika waraka wake wa pili. Katika waraka huu Paulo anaeleza hisia zake,
wajibu, shauku na majukumu katika hali ya majadiliano katika ushirika wa Wakorintho wenyewe na mashambulizi
yaliyokuwa yameelekezwa kwake binafsi kama mtume. Katika kushughulikia matatizo hayo, katika waraka huu
wa pili Paulo alitaka kuthibitisha mamlaka yake. Kulikuwa na mashaka makubwa katika kanisa hilo kumhusu,
japokuwa hatuelewi ni kwa nini. Lakini Paulo anaandika kwa uchungu mkubwa, kuthibitisha mamlaka yake kama
mtume. Anajaribu pia kushughulikia masuala ya kiutekelezaji hasa kuhusu kusaidia waamini wasiojiweza walioko
sehemu nyingine.
Wazo Kuu
Katika barua hii Paulo anaonyesha jinsi tunavyoweza kupata ushindi katika mateso. Barua hii ni ya binafsi.
Inaandikwa na mtu aliyekosewa sana na watu aliowapenda sana. Paulo anapoorodhesha mambo aliyoyapitia
katika maisha yake kama mtumishi wa Kristo, tunaona jinsi neema ya Mungu inavyotenda kazi, ikileta mema
kutoka katika mateso. Shetani anafanya bidii kujaribu kuiharibu kazi ya Mungu lakini Mungu ni mshindi na
anawainua wale wanaomtegemea.
Mwandishi
Paulo
Mahali
Paulo aliandika waraka huu akiwa Makedonia baada ya kumaliza huduma yake ya miaka miwili huko Efeso.
Tarehe
Waraka huu unaotambuliwa kama 2Wakorinthio inaonekana uliandikwa miezi michache tu baada ya ule wa
kwanza, yamkini kabla tu ya kuanza kwa majira ya baridi katika mwaka 55 B.K.
Mgawanyo
Salamu na utambulisho (1:1-9)
Mashindano ya makundi ndani ya kanisa (1:10 - 4::21)
Uasherati, kushtakiana, usafi katika mwili (5:1- 6:20)
Ndoa na useja ( 7:1- 40)
Haki za Mkristo na wajibu wake (8:1-11:1)
Mkristo katika ibada ya hadhara (11:2 - 34)
Nafasi na umuhimu wa karama za Roho (12:1-14 :40).
Ufufuo – msingi wa Imani ya Kikristo (15:1- 58)
Hitimisho (16:1- 24)
1
2Wakorinto
Salamu
Barua hii ni kutoka kwangu mimi, Paulo,
mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya
Mungu na Timotheo ndugu yetu,
kuelewa kwa ukamilifu ili mweze kujivuna kwa
ajili yetu, kama na sisi tutakavyojivuna kwa ajili
yenu katika siku ya Bwana Yesu.
15 Kwa kuwa nilikuwa na uhakika wa mambo
haya, nilitaka nije kwenu kwanza, ili mpate
upendeleo mara mbili. 16 Nilipanga
kuwatembelea nikiwa safarini kwenda
Makedonia na kurudi tena kwenu nikitoka
Makedonia, ili mnisafirishe katika safari yangu
ya kwenda Uyahudi. 17 Nilipopanga jambo hili, je,
nilikuwa kigeugeu ? Au ninafanya mipango
yangu kidunia, ili niseme, “Ndiyo, ndiyo’’ na
“Siyo, siyo’’ wakati huo huo ?
18 Hakika kama Mungu alivyo mwaminifu,
maneno yetu kwenu hayajawa “Ndiyo na Siyo’’.
19 Kwa kuwa Mwana wa Mungu Yesu Kristo,
ambaye tulimhubiri kwenu mimi, Silvano na
Timotheo, hakuwa ‘‘Ndiyo’’ na ‘‘Siyo’’, bali katika
Yeye sikuzote ni “Ndiyo’’. 20 Kwa maana ahadi
zote za Mungu zilizo katika Kristo ni “Ndiyo”.
Kwa sababu hii ni katika Yeye tunasema
“Amen” kwa utukufu wa Mungu. 21 Basi ni Mungu
atufanyaye sisi pamoja nanyi kusimama imara
katika Kristo. Ametutia mafuta 22 kwa kututia
muhuri Wake na kutupa Roho wake mioyoni
mwetu kuwa rehani kwa ajili ya kututhibitishia
kile kijacho.
23 Mungu ni shahidi yangu kwamba ilikuwa ni
kwa kuwahurumia sikurudi Korintho. 24 Si
kwamba tunatawala imani yenu, bali twatenda
kazi pamoja nanyi kwa ajili ya furaha yenu, kwa
abu ni kwa imani mwasimama imara.
1
Kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho,
pamoja na watakatifu wote walioko Akaya yote:
2 Neema na amani kutoka kwa Mungu Baba
yetu na Bwana Yesu Kristo iwe nanyi.
Mungu Wa Faraja Yote
3 Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu
Yesu Kristo, Baba wa huruma na Mungu wa
faraja yote. 4 Yeye atufarijiye katika taabu zetu
zote, ili tuweze kuwafariji wale walio katika
taabu yo yote kwa faraja ambayo sisi wenyewe
tumepokea kutoka kwa Mungu. 5 Kama vile
mateso ya Kristo yanavyotitirika ndani ya
maisha yetu, hivyo ndivyo faraja yetu
inavyofurika kwa njia ya Kristo. 6 Kama
tunataabika, ni kwa ajili ya faraja na wokovu
wenu, kama tukifarijiwa, ni kwa ajili ya faraja
yenu, iwaleteayo saburi ya mateso yale yale
yanayotupata. 7 Nalo tumaini letu kwenu ni
thabiti, kwa sababu tunajua kwamba kama vile
mnavyoshiriki
mateso
yetu,
ndivyo
pia
mnavyoshiriki katika faraja yetu.
8 Ndugu wapendwa, hatutaki msijue kuhusu
zile taabu tulizopata huko Asia. Kwa maana
tulilemewa na mizigo sana kiasi cha kushindwa
kuvumilia, kwamba hata tulikata tamaa kuishi.
9 Kwa kweli, mioyoni mwetu tulihisi tumekabiliwa
na hukumu ya kifo, ili tusijitegemee sisi
wenyenye bali tumtegemee Mungu afufuaye
wafu. 10 Yeye aliyetuokoa kwenye hatari kubwa
ya kifo ataendelea kutuokoa. Kwake Yeye
tumeweka tumaini letu kwamba atatuokoa tena.
11 Kama vile mlivyoungana kusaidiana nasi
katika maombi, hivyo wengi watatoa shukrani
kwa niaba yetu kwa ajili ya baraka tulizopata
kwa maombi ya wengi.
sab
2
Hivyo nilikusudia moyoni mwangu
nisifanye ziara nyingine yenye kuwaumiza
ninyi. 2 Kwa kuwa kama nikiwahuzunisha ninyi,
ni nani aliyebaki wa kunifurahisha isipokuwa
ninyi ambao nimewahuzunisha? 3 Niliandika
hivyo kama nilivyofanya, ili nikija nisihuzunishwe
na wale watu ambao wangenifanya nifurahi.
Nina imani na ninyi nyote, kwamba wote
ningeshiriki furaha yangu. 4 Kwa maana
niliwaandikia katika dhiki kubwa na kutaabika
sana moyoni tena kwa machozi mengi, shabaha
yangu si ili niwasababishe mhuzunike bali
kuwaonyesha kina cha upendo wangu kwenu.
Msamaha Kwa Mwenye Dhambi
5 Basi ikiwa mtu ye yote amesababisha
huzuni, kwa kiasi fulani hakunihuzunisha mimi
kama alivyowahuzunisha ninyi nyote, ili
nisiifanye kali kupita kiasi. 6 Adhabu hii
aliyopewa na wengi inamtosha. 7 Basi sasa
badala yake, inawapasa kumsamehe na
Paulo Ahairisha Ziara
12 Basi haya ndiyo majivuno yetu: Dhamiri
yetu inatushuhudia kwamba tumeenenda katika
ulimwengu na hasa katika uhusiano wetu na
ninyi, katika utakatifu na uaminifu utokao kwa
Mungu. Hatukufanya hivyo kwa hekima ya
kidunia bali kwa neema ya Mungu. 13 Kwa
maana hatuwaandikii mambo ambayo hamwezi
kusoma au kuyaelewa. Natumaini kwamba,
14 kama vile mlivyotuelewa kwa sehemu, mtakuja
2
952117691.003.png
 
2Wakorinto
kumfariji, ili asigubikwe na huzuni kupita kiasi.
8 Kwa hiyo, nawasihi, mpate kuuthibitisha tena
upendo wenu kwa ajili yake. 9 Sababu ya
kuwaandikia ni kuona kama mngeweza
kushinda hilo jaribio na kutii katika kila jambo.
10 Kama ninyi mkimsamehe mtu ye yote, mimi
pia nimemsamehe. Kile nilichosamehe, kama
kulikuwa na kitu cho chote cha kusamehe,
nimekwisha kusamehe mbele ya Kristo kwa ajili
yenu. 11 Ili Shetani asitushinde. Kwa maana
hatuachi kuzijua hila zake.
kwa kuwa andiko huua bali Roho hutia uzima.
Utukufu Wa Agano Jipya
7 Basi ikiwa ile huduma iliyoleta mauti, ile
iliyoandikwa kwa herufi juu ya jiwe ilikuja kwa
utukufu hata ikawa Waisraeli hawawezi
kuutazama uso wa Mose kwa sababu ya ule
utukufu wake, ingawa ulikuwa ni wa kufifia, 8 je,
huduma ya Roho haitakuwa na utukufu zaidi?
9 Ikiwa huduma ile iwahukumuyo wanadamu ina
utukufu, si itakuwa ya utukufu zaidi ile huduma
iletayo haki? 10 Kwa maana kile kilichokuwa na
utukufu sasa hakina utukufu ukilinganisha na
huu utukufu uzidio sana wa Agano Jipya.
11 Ikiwa kile kilichokuwa kinafifia kilikuja kwa
utukufu, si zaidi sana ya utukufu wa kile
kinachodumu?
12 Kwa hiyo, kwa kuwa tunalo tumaini hili,
tuna ujasiri sana. 13 Sisi si kama Mose, ambaye
ilimpasa kuweka utaji ili kufunika uso wake
Waisraeli wasiuone ule mng'ao ulivyokuwa juu
yake wakati ukififia na hatimaye kutoweka.
14 Lakini akili zao zilitiwa upumbavu, kwa maana
mpaka leo utaji ule ule hufunika wakati Agano la
Kale lisomwapo.Huo utaji haujaondolewa kwa
maana ni katika Kristo peke Yake unaondolewa.
15 Hata leo, torati ya Mose isomwapo, utaji
hufunika mioyo yao. 16 Lakini wakati wo wote
mtu anapomgeukia Bwana, “utaji
unaondolewa.’’ 17 Basi Bwana ndiye Roho.
Mahali alipo Roho wa Bwana hapo pana uhuru.
18 Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji
tunaakisi utukufu wa Bwana, kama kwenye kioo.
Nasi tunabadilishwa ili tufanane naye, toka
utukufu hadi utukufu mkuu zaidi, utokao kwa
Bwana, ambaye ndiye Roho.
Wasiwasi Wa Paulo Huko Troa
12 Basi nilipofika Troa kuhubiri Injili ya Kristo
na kukuta kwamba Bwana alikuwa
amenifungulia mlango, 13 bado nilikuwa sina
utulivu akilini mwangu kwa sababu sikumkuta
ndugu yangu Tito huko. Hivyo niliagana nao
nikaenda Makedonia.
14 Lakini Mungu ashukuriwe, Yeye ambaye
sikuzote hutufanya tuandamane kwa ushindi
tukiwa ndani ya Kristo. Naye kwa kutupitia sisi
hueneza kila mahali kama harufu nzuri ya
kumjua Yeye. 15 Kwa maana sisi kwa Mungu ni
harufu nzuri ya manukato ya Kristo miongoni
mwa wale wanaookolewa. 16 Kwa wale
wanaopotea sisi ni harufu ya mauti, lakini kwa
wale wanaookolewa sisi ni harufu nzuri iletayo
uzima. Ni nani basi awezaye kazi hiyo? 17 Tofauti
na watu wengine wengi, sisi hatuchuuzi neno la
Mungu kwa ajili ya kupata faida. Kinyume
chake, katika Kristo tunalisema neno la Mungu
kwa unyofu, kama watu tuliotumwa kutoka kwa
Mungu.
Wahudumu Wa Agano Jipya
Je, tunaanza kujisifu wenyewe tena? Au
tunahitaji kupata barua za utambulisho
kwenu au kutoka kwenu, kama watu wengine?
2 Ninyi wenyewe ndio barua yetu iliyoandikwa
katika mioyo yetu, inayojulikana na kusomwa na
kila mtu. 3 Nanyi mwadhihirisha wazi kwamba
ninyi ni barua itokayo kwa Kristo, matokeo ya
huduma yetu, ambayo haikuandikwa kwa wino
bali kwa Roho wa Mungu aliye hai, si katika
vibao vya mawe, bali katika vibao ambavyo ni
mioyo ya wanadamu.
4 Hili ndilo tumaini tulilo nalo mbele za
Mungu kwa njia ya Kristo. 5 Si kwamba sisi
tunafikiri kuwa tunaweza kufanya jambo lo lote
wenyewe, lakini nguvu yetu inatoka kwa Mungu.
6 Yeye ndiye aliyetufanya sisi kuwa wahudumu
wa Agano Jipya, si wa andiko bali wa Roho,
3
Hazina Ya Mbinguni Kwenye Vyombo Vya
Udongo
Kwa hiyo, kwa kuwa tuna huduma hii kwa
rehema za Mungu, hatukati tamaa.
2 Tumekataa mambo ya siri na ya aibu, wala
hatufuati njia za udanganyifu, tukichanganya
Neno la Mungu na uongo. Kinyume cha hayo
kwa kudhihirisha kweli waziwazi na
kujitambulisha wenyewe kwenye dhamiri ya kila
mtu mbele za Mungu. 3 Hata nayo Injili yetu
kama imetiwa utaji, ni kwa wale tu wanaopotea.
4 Kwa habari yao, mungu wa dunia hii
amepofusha akili za wasioamini, ili wasione
nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo, aliye sura ya
Mungu. 5 Kwa maana hatujihubiri sisi wenyewe
ila tunamhubiri Yesu Kristo kuwa ni Bwana na
4
3
952117691.004.png
 
2Wakorinto
sisi ni watumishi wenu kwa ajili ya Yesu. 6 Kwa
kuwa Mungu, Yeye aliyesema, ‘‘Nuru na ing’ae
gizani,’’ ameifanya nuru Yake ing’ae mioyoni
mwetu ili kutupatia nuru ya maarifa ya utukufu
wa Mungu katika uso wa Kristo.
7 Lakini tunayo hazina hii katika vyombo vya
udongo, ili ijulikane wazi kwamba uwezo huu wa
ajabu unatoka kwa Mungu wala si kwetu.
8 Twataabika kila upande, lakini hatuangamizwi,
twaona wasiwasi lakini hatukati tamaa,
9 twateswa lakini hatuachwi, twatupwa chini
lakini hatupondwi. 10 Sikuzote twachukua katika
mwili kufa Kwake Yesu ili kwamba uzima wa
Yesu uweze kudhihirika katika miili yetu. 11 Kwa
maana sisi tulio hai sikuzote tumetolewa tufe
kwa ajili ya Yesu, ili kwamba uzima wake upate
kudhihirishwa katika mwili wetu upatikanayo na
mauti. 12 Hivyo basi, mauti inatenda kazi ndani
yetu, bali uzima unatenda kazi ndani yenu.
13 Imeandikwa, ‘‘Niliamini, kwa hiyo
nimesema.’’ Kwa roho yule yule wa imani pia
tuliamini na hivyo tukasema, 14 kwa sababu
tunajua kwamba Yeye aliyemfufua Bwana Yesu
kutoka kwa wafu atatufufua pia na sisi pamoja
na Yesu na kutuleta sisi pamoja nanyi mbele
Zake. 15 Haya yote ni kwa faida yenu, ili kwamba
neema ile inavyowafikia watu wengi zaidi na
zaidi, ipate kusababisha shukrani nyingi kwa
utukufu wa Mungu.
16 Kwa hiyo, hatukati tamaa. Ingawa utu
wetu wa nje unachakaa, utu wetu wa ndani
unafanywa upya siku kwa siku. 17 Kwa maana
dhiki yetu nyepesi iliyo ya kitambo
inatutayarisha kwa ajili ya utukufu wa milele
uzidio kuwa mwingi kupita kiasi, 18 kwa sababu
hatuangalii yale yanayoweza kuonekana bali
yale yasiyoweza kuonekana, kwa maana yale
yanayoweza kuonekana ni ya kitambo tu, bali
yale yasiyoweza kuonekana ni ya milele.
aliyetufanya kwa ajili ya jambo ilo hilo naye
ametupa Roho Mtakatifu kuwa amana,
akituahidia kile kijacho.
6 Kwa hiyo sikuzote tunalo tumaini, hata
ingawa tunajua kwamba wakati tukiwa katika
mwili huu, tuko mbali na Bwana, 7 kwa maana
twaenenda kwa imani wala si kwa kuona.
8 Naam, tunalo tumaini na ingekuwa bora zaidi
kuuacha mwili huu na kwenda kukaa na Bwana.
9 Kwa hiyo, kama tuko katika mwili huu au tuko
mbali nao, lengo letu ni kumpendeza Bwana.
10 Kwa kuwa sisi sote tutasimama mbele ya kiti
cha hukumu cha Kristo, ili kila mmoja apate
kulipwa kwa ajili ya yale ambayo yametendwa
katika mwili wake, yakiwa mema au mabaya.
Huduma Ya Upatanisho
11 Basi, kwa kuwa tunajua kumcha Bwana,
tunajitahidi kuwavuta wengine, lakini Mungu
anatufahamu dhahiri, nami natumaini kwamba
tu dhahiri katika dhamiri zenu pia. 12 Sio kwamba
tunajaribu kujistahilisha kwenu tena, lakini
tunataka kuwapa nafasi ili mwone fahari juu
yetu mweze kuwajibu hao wanaoona fahari juu
ya mambo yanayoonekana badala ya mambo
yaliyo moyoni. 13 Kama tumerukwa na akili, ni
kwa ajili ya Mungu, kama tuna akili timamu ni
kwa ajili yenu. 14 Kwa kuwa upendo wa Kristo
unatutia nguvu, kwa sababu tunasadiki kuwa
mmoja alikufa kwa ajili ya wote, kwa hiyo wote
walikufa. 15 Naye alikufa kwa ajili ya watu wote,
ili kwamba wote wanaoishi wasiishi tena kwa
ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili Yake
Yeye aliyekufa na kufufuka tena kwa ajili yao.
16 Hivyo tangu sasa hatumwangalii mtu ye
yote kwa mtazamo wa kibinadamu, ingawa
wakati fulani tulimwangalia Kristo kwa namna ya
kibinadamu, hatumwangalii tena kwa jinsi hiyo.
17 Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo,
amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita,
tazama, yamekuwa mapya. 18 Haya yote
yanatokana na Mungu, ambaye ametupatanisha
sisi na nafsi yake kwa njia ya Yesu Kristo na
kutupatia sisi huduma ya upatanisho: 19 Kwamba
Mungu alikuwa ndani ya Kristo akiupatanisha
ulimwengu na nafsi Yake mwenyewe, akiwa
hawahesabii watu dhambi zao. Naye
ametukabidhi sisi ujumbe huu wa upatanisho.
20 Kwa hiyo sisi ni mabalozi wa Kristo, kana
kwamba Mungu anawasihi kwa kupitia vinywa
vyetu, nasi twawaomba sana ninyi kwa niaba ya
Kristo, mpatanishwe na Mungu. 21 Kwa maana
Mungu alimfanya Yeye asiyekuwa na dhambi
Mak
ao Yetu Ya Mbinguni
5
Kwa maana twajua kwamba kama hema
yetu ya dunia tunayoishi ikiharibiwa,
tunalo jengo kutoka kwa Mungu, nyumba
isiyojengwa kwa mikono ya wanadamu. 2 Kwa
maana katika hema hii twalia kwa uchungu,
tukitamani kuvikwa makao yetu ya mbinguni,
3 kwa kuwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tena
kuwa uchi. 4 Kwa kuwa tukiwa bado katika hema
hii twalia kwa uchungu na kulemewa, kwa
sababu hatutaki kuvuliwa bali kuvikwa makao
yetu ya mbinguni ili kwamba kile kipatikanacho
na mauti kimezwe na uzima. 5 Basi Mungu ndiye
4
952117691.001.png
 
2Wakorinto
kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate
kufanywa haki ya Mungu katika Yeye.
Kama watenda kazi pamoja na Mungu,
tunawasihi msipokee neema ya Mungu
bure bila sababu . 2 Kwa maana asema:
katikati yao, nami nitakuwa Mungu wao, nao
watakuwa watu wangu.’’
17 ‘‘Kwa hiyo tokeni miongoni mwao,
mkatengwe nao,
asema Bwana.
Msiguse kitu cho chote kilicho najisi,
Nami nitawakaribisha.’’
18 ‘‘ Mimi nitakuwa Baba kwenu,
6
“Wakati uliokubalika nilikusikia,
siku ya wokovu nilikusaidia.’’
Tazama, wakati uliokubalika ndio huu, siku ya
wokovu ndiyo sasa.’’
nanyi mtakuwa wanangu na binti zangu,
asema Bwana Mwenyezi.’’
7
Taabu Za Paulo
3 Hatuweki kitu cha kukwaza katika njia ya
mtu ye yote, ili huduma yetu isionekane kuwa
na lawama, 4 bali kama watumishi wa Mungu
tuonyeshe kwa kila njia saburi nyingi katika
dhiki, katika misiba, katika shida, 5 katika
kupigwa, katika kufungwa gerezani na katika
ghasia, katika kazi ngumu, katika kukesha na
katika njaa, 6 katika utakatifu, katika ufahamu,
katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho
Mtakatifu na upendo wa kweli, 7 katika maneno
ya kweli na katika nguvu za Mungu, kwa silaha
za haki za mkono wa kuume na za mkono za
kushoto, 8 katika utukufu na katika kudharauliwa,
katika sifa mbaya na katika sifa nzuri, kama
wadanganyaji lakini tukiwa wakweli 9 tukiwa
maarufu lakini tukihesabiwa kama tusiojulikana,
tukiwa kama wanaokufa lakini tunaishi,
tukipigwa lakini hatuuawi, 10 kama wenye huzuni
lakini sikuzote tukifurahi, tukionekana maskini
lakini tukitajirisha wengi, tukiwa kama wasio na
kitu lakini tukiwa na vitu vyote.
11 Tumesema nanyi wazi, enyi Wakorintho
na kuwafungulieni mioyo yetu wazi kabisa. 12 Sisi
hatujizuii kuwapenda, bali ninyi mmeuzuia
upendo wenu kwetu. 13 Sasa nasema, kama na
watoto wangu: Ninyi pia
ifungueni mioyo yenu kabisa.
Wapenzi, kwa kuwa tunazo ahadi hizi,
basi na tujitakase nafsi zetu kutokana na
kila kitu kitiacho mwili na roho unajisi, tukitimiza
utakatifu kwa kumcha Mungu.
Furaha Ya Paulo
2 Tupatieni nafasi mioyoni mwenu.
Hatujamkosea mtu ye yote, hatujampotosha mtu
ye yote, wala hatujamdhulumu mtu ye yote.
3 Sisemi haya ili kuwahukumu, kwa kuwa
nilisema mwanzo, kwamba ninyi mko mioyoni
mwetu hata kwa kufa pamoja au kuishi pamoja.
4 Mara nyingi najivuna kwa ajili yenu, naona
fahari juu yenu, nimejawa na faraja, nina furaha
kupita kiasi katika mateso yetu yote.
5 Kwa maana hata tulipoingia Makedonia,
miili yetu haikuwa na raha. Tulisumbuliwa kila
upande, kwa nje kulikuwa na mapigano na
mioyoni mwetu tulikuwa na hofu. 6 Bali Mungu,
Yeye awafarijie wenye huzuni, alitufariji kwa
kufika kwake Tito, 7 lakini si kule kuja kwa Tito
tu, bali pia kwa faraja mliyompa. Alitueleza jinsi
mlivyomwonea shauku, huzuni yenu kubwa na
juhudi yenu kwa ajili yangu, ili kwamba furaha
yangu ipate kuwa kubwa kuliko wakati wo wote.
8 Hata kama niliwahuzunisha kwa barua
yangu, sijutii. Ingawa nilijuta kwa muda mfupi,
kwa kuwa najua kwamba barua yangu
iliwaumiza, lakini ni kwa kitambo tu, 9 Lakini sasa
nina furaha, si kwa sababu mlihuzunika, bali
kwa kuwa huzuni hiyo iliwafanya mtubu. Kwa
maana mlihuzunishwa kama Mungu
alivyokusudia watu wahuzunike na hivyo sisi
hatukuwadhuru kwa njia yo yote. 10 Kwa maana
huzuni ya kimungu huleta toba iletayo wokovu
na wala haina majuto. Lakini huzuni ya kidunia
husababisha mauti. 11 Tazameni jinsi huzuni hii
ya kimungu ilivyoleta faida kutokana na huzuni
hii: bidii mliyo nayo, juhudi mliyofanya kujitetea,
uchungu wenu, hofu yenu, upendo wenu,
shauku yenu na jinsi mlivyokuwa tayari kutoa
Msifungiwe Nira Pamoja Na Wasioamini
14 Msifungiwe nira pamoja na watu
wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa, kwa
maana pana uhusiano gani kati ya haki na
uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na
giza? 15 Kuna mapatano gani kati ya Kristo na
Beliali a ? Yeye aaminiye ana sehemu gani na
yeye asiyeamini? 16 Kuna mapatano gani kati ya
hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi tu
hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu
alivyosema : ‘‘Nitakaa pamoja nao na kutembea
a 15 Beliali hapa ina maana ya “uovu”, “kutokumcha Mungu”
5
952117691.002.png
 
Zgłoś jeśli naruszono regulamin