1KI_Kiswahili_1068.pdf

(307 KB) Pobierz
1 WAFALME
Utangulizi
Katika andiko la Kiebrania, vitabu vya 1Wafalme na 2Wafalme vinahesabiwa kuwa ni kitabu kimoja
kinachoitwa “Wafalme” katika mapokeo ya Kiyahudi. Huku kutenganishwa kwa vitabu hivi kulifanywa na watafsiri
wa Agano la Kale la Kiyunani “Septuagint”na kuvitambulisha kama “Kitabu cha Tatu na cha Nne cha Wafalme.
Kitabu hiki kinaanzia utawala wa Solomoni (1046K.K – 616K.K.) na kuelezea habari za Israeli mpaka kufikia kifo
cha Mfalme Ahazia mwana wa Ahabu. ( 3:1 – 11:43) kinaelezea utawala wa Solomoni, ikiwa ni pamoja na ujenzi
wa hekalu na jumba la kifalme katika Yerusalemu.
Rehoboamu, mwana wa Solomoni alichukua ufalme baada ya kifo cha Solomoni baba yake, lakini sehemu
ya kaskazini ilichukuliwa na Yeroboamu aliyekuwa mtumishi wa Sauli. Baada ya mgawanyiko huu, upande wa
kaskazini uliitwa Israeli na ule wa kusini ukaitwa Yuda. Sura za mwisho za 1Wafalme,zinazungumzia habari za
mfalme mwovu Ahabu aliyekuwa amemwoa Yezebeli, mtumishi wa Baali na Eliya nabii wa Mungu ambaye
alikemea uovu wa Ahabu na kutokutii kwa Israeli.Kipindi hiki Israeli walimwacha BWANA na kuabudu Baali.
Kwa kuwa mwandishi wa 1 na 2Wafalme alivutiwa zaidi kuhusu suala la uaminifu wa Israeli kwa Mungu na
agano lake, aliandika kuhusu kila mfalme kuonyesha jinsi alivyokuwa mwaminifu au jinsi alivyomwasi Mungu.
Mara kwa mara mwandishi alitumia maneno, ‘‘Alifanya yaliyo maovu machoni pa Mungu,’’ ili kuelezea uovu wa
mfalme mhusika au, “Alifanya yaliyo mema machoni pa Mungu,’’ kuelezea uadilifu wa mfalme mhusika.
Kama ilivyo katika Walawi, mwandishi anaandika kwamba, wakati Israeli walipomtii Mungu, alileta amani
katika nchi, lakini walipoacha kumtii na kuabudu sanamu, nchi ya Israeli iliathirika kwa vita na maafa mengine.
Mwandishi
Inasemekana labda ni Isaya na Yeremia ndio walioandika au waliofanya makusanyo ya mwisho kwa kutumia
kumbukumbu za wafalme wa Israeli. Waliohusika kuandika kumbukumbu hizo walikuwa Nathani, Godi, Ido,
Ahiya, Yehu na wengine. Mapokeo ya Kiyahudi yanasema Yeremia ndiye mwandishi. Inaelekea kutokana na
2Mambo ya Nyakati 32:32 kwamba Isaya ndiye mwandishi hadi wakati wa Mfalme Hezekia, naye Yeremia
akamalizia akieleza matukio kuanzia hapo hadi wakati wa uhamisho.
Mahali
Kitabu hiki kiliandikwa katika nchi ya Palestina. Taifa la Israeli ambalo lilikuwa taifa moja kubwa, sasa
limegawanyika. Siyo tu kijeografia lakini pia kiroho.Sasa panakuwa na taifa la kaskazini –Israeli na la kusini –
Yuda.
Tarehe
1046 -616 K. K.
Wahusika Wakuu
Daudi, Solomoni, Rehoboamu, Yeroboamu, Abiya, Asa, Eliya, Ahabu na Yezebeli.
Mgawanyo
Utawala wa Solomoni. (1:1-11:43)
Rehoboamu na Yeroboamu. (12:1-14:31)
Wafalme wa Israeli na Yuda. (15:1-16:34 )
Eliya na Ahabu. (17:1-19:21)
Utawala wa Ahabu na Yezebeli. (20:1-22:53)
1
1 WAFALME
Adonia Ajitangaza Mwenyewe Kuwa Mfalme
Mfalme Daudi alipokuwa mzee umri ukiwa
umesogea, hakuweza kupata joto hata
walipomfunika kwa nguo. 2 Kwa hiyo watumishi
wake wakamwambia, “Turuhusu tumtafute
kijana mwanamwali bikira amhudumie mfalme
na kumtunza. Anaweza kulala pembeni mwake
ili bwana wetu mfalme apate joto.”
3 Kisha wakatafuta katika Israeli yote ili
kumpata msichana mzuri wa sura na
wakampata Abishagi, Mshunami, wakamleta
kwa mfalme. 4 Msichana huyo alikuwa mzuri
sana wa sura, akamtunza mfalme na
kumhudumia, lakini mfalme hakufanya naye
tendo la ndoa.
5 Basi Adonia, ambaye mama yake alikuwa
Hagithi, akajigamba na kusema, “Mimi nitakuwa
mfalme.” Hivyo akajiwekea tayari magari na
wapanda farasi, pamoja na watu hamsini
watakaomtangulia wakikimbia. 6 (Baba yake
hakuwa ameingilia na kumwuliza, “Kwa nini
unafanya hivyo?” Alikuwa pia kijana mzuri sana
wa sura na alizaliwa baada ya Absalomu.)
7 Adonia akashauriana pamoja na Yoabu
mwana wa Seruya na kuhani Abiathari, nao
wakamsaidia. 8 Lakini kuhani Sadoki, Benaya
mwana wa Yehoyada, Nathani nabii, Shimei, Rei
na walinzi maalumu wa Daudi hawakujiunga na
Adonia.
9 Ndipo Adonia akatoa dhabihu ya kondoo,
ng'ombe na ndama walionona kwenye Jiwe la
Zohelethi karibu na En Rogeli. Akawaalika
ndugu zake wote, wana wa mfalme na wanaume
wote wa Yuda waliokuwa maafisa wa kifalme,
10 lakini hakumwalika nabii Nathani, Benaya,
walinzi maalumu wa mfalme wala ndugu yake
Solomoni.
11 Ndipo Nathani akamwuliza Bathsheba,
mama yake Solomoni, “Je, hujasikia kwamba
Adonia, mwana wa Hagathi, amekuwa mfalme
pasipo bwana wetu Daudi kujua jambo hili?
12 Sasa basi, acha nikushauri jinsi utakavyookoa
uhai wako mwenyewe na uhai wa mwanao
Solomoni. 13 Ingia kwa Mfalme Daudi na
umwambie, ‘Bwana wangu mfalme, je
hukuniapia mimi mtumishi wako: “Hakika
mwanao Solomoni atakuwa mfalme baada
yangu na ndiye atakayeketi juu ya kiti changu
cha ufalme?’’ Kwa nini basi Adonia amekuwa
mfalme?’
15 Hivyo Bath-sheba akaenda kumwona
mfalme aliyekuwa mzee chumbani mwake
mahali ambapo Abishagi Mshunami alikuwa
akimhudumia. 16 Bath-sheba akasujudu na
kupiga magoti mbele ya mfalme.
1
Mfalme akauliza, “Ni nini hiki unachotaka?’’
17 Akamwambia, “Bwana wangu, wewe
mwenyewe uliniapia mimi mtumishi wako kwa
BWANA wa ko kwamba: ‘Solomoni Mwanao
atakuwa mfalme baada yangu na ndiye
atakayeketi kwenye kiti changu cha ufalme.’
18 Lakini sasa Adonia amekuwa mfalme, nawe,
bwana wangu mfalme huna habari kuhusu
jambo hilo. 19 Ametoa dhabihu idadi kubwa ya
ng'ombe, ndama walionona na kondoo, naye
amewaalika wana wa mfalme wote, kuhani
Abiathari na Yoabu jemadari wa jeshi, lakini
hakumwalika Solomoni mtumishi wako. 20 Bwana
wangu mfalme, macho ya Israeli yote
yanakutazama wewe wajue kutoka kwako kuwa
ni nani atakayeketi katika kiti cha ufalme cha
bwana wangu mfalme baada yake. 21 Kama
sivyo, mara tu bwana wangu mfalme
atakapopumzishwa pamoja na baba zake, mimi
na mwanangu Solomoni tutatendewa kama
wahalifu.’’
22 Alipokuwa angali anazungumza na
mfalme, nabii Nathani akafika. 23 Wakamwambia
mfalme, “Nabii Nathani yuko hapa.’’ Kisha
akaenda mbele ya mfalme na kumsujudia hadi
uso wake ukagusa ardhi.
24 Nathani akasema, “Je, bwana wangu
mfalme, umetangaza kuwa Adonia atakuwa
mfalme baada yako na kwamba ataketi kwenye
kiti chako cha ufalme? 25 Leo ameshuka na kutoa
dhabihu idadi kubwa ya ng'ombe, ndama
walionona na kondoo. Amewaalika wana wote
wa mfalme, jemadari wa jeshi na kuhani
Abiathari. Sasa hivi, wanakula na kunywa
pamoja naye wakisema, ‘Aishi maisha marefu
Mfalme Adonia!’ 26 Lakini mimi mtumishi wako,
kuhani Sadoki, Benaya mwana wa Yehoyada na
mtumishi wako Solomoni hakutualika. 27 Je, hili ni
jambo ambalo bwana wangu mfalme amelifanya
pasipo kuwajulisha watumishi wake ili wapate
kujua ni nani atakayeketi kwenye kiti cha ufalme
cha bwana wangu mfalme baada yake?’’
Daudi Amfanya Solomoni Kuwa Mfalme
28 Ndipo mfalme Daudi akasema, “Mwite
Bath-sheba, aingie ndani.’’ Hivyo akaingia mbele
ya mfalme na kusimama mbele yake.
14 Utakapokuwa ukizungumza na
mfalme,
nitaingia
na
kuthibitisha
hayo
uliyoyasema.’’
2
952102164.003.png
 
1 WAFALME
29 Ndipo mfalme akaapa: “Hakika kama
BWANA aishivyo, ambaye ameniokoa kutoka
katika kila taabu, 30 hakika nitatekeleza leo kile
nilichokuapia kwa BWANA wa Israeli: Mwanao
Solomoni atakuwa mfalme baada yangu, naye
ataketi kwenye kiti changu cha ufalme baada
yangu.’’
31 Kisha Bathsheba akasujudu akipiga
magoti mbele ya mfalme uso wake ukigusa ardhi
akasema, “Bwana wangu Mfalme Daudi na aishi
milele!’’
32 Mfalme Daudi akasema, “Mwite kuhani
Sadoki ndani, nabii Nathani na Benaya mwana
wa Yehoyada.’’ Walipofika mbele ya mfalme,
33 akawaambia: “Wachukueni watumishi wa
bwana wenu pamoja nanyi na mkamkalishe
mwanangu Solomoni juu ya nyumbu wangu
mwenyewe mkamtelemshe hadi Gihoni. 34 Huko
kuhani Sadoki na nabii Nathani wamtie mafuta
awe mfalme juu ya Israeli. Pigeni tarumbeta na
mpaze sauti, ‘Mfalme Solomoni aishi maisha
marefu!’ 35 Kisha mtapanda pamoja naye,
atakuja na kuketi kwenye kiti changu cha ufalme
na kutawala badala yangu. Nimemweka awe
mtawala juu ya Israeli na Yuda.”
36 Benaya mwana wa Yehoyada akamjibu
mfalme, “Amen! BWANA wa bwana wangu
mfalme na aseme vivyo hivyo. 37 Kama vile
BWANA alivyokuwa na bwana wangu mfalme,
vivyo hivyo na awe na Solomoni
kukifanya kiti chake cha utawala kuwa kikuu
kuliko kile cha bwana wangu Mfalme Daudi!’’
38 Hivyo kuhani Sadoki, nabii Nathani,
Benaya mwana Yehoyada, Wakerethi na
Wapelethi wakampandisha Solomoni juu ya
nyumbu wa Mfalme Daudi nao wakamsindikiza
hadi Gihoni. 39 Kuhani Sadoki akachukua pembe
ya mafuta kutoka kwenye hema takatifu na
kumtia Solomoni mafuta. Kisha wakapiga
tarumbeta na watu wote wakapaza sauti
wakisema, “Mfalme Solomoni aishi maisha
marefu!’’ 40 Na watu wote wakakwea wakimfuata,
wakipiga filimbi na kushangilia sana, hata ardhi
ikatikisika kwa ile sauti.
41 Adonia pamoja na wageni wote waliokuwa
pamoja naye wakasikia sauti hiyo walipokuwa
wakimalizia karamu yao. Waliposikia sauti ya
tarumbeta, Yoabu akauliza, “Nini maana ya
makelele yote haya katika mji?’’
42 Hata alipokuwa anasema, Yonathani
mwana wa kuhani Abiathari akafika. Adonia
akasema, “Ingia ndani, mtu mstahiki kama wewe
ni lazima alete habari njema.’’
43 “Yonathani akajibu, “La hasha! Mfalme
Daudi bwana wetu amemfanya Solomoni kuwa
mfalme. 44 Mfalme amemtuma pamoja naye
kuhani Sadoki, nabii Nathani, Benaya mwana
wa Yehoyada, Wakerethi na Wapelethi nao
wamempandisha juu ya nyumbu wa mfalme,
45 nao kuhani Sadoki na nabii Nathani wamemtia
mafuta kuwa mfalme huko Gihoni. Kuanzia hapo
wameendelea kushangilia na sauti zimeenea
pote mjini. Hizo ndizo kelele unazosikia. 46 Zaidi
ya hayo, Solomoni ameketi juu ya kiti chake cha
ufalme. 47 Pia, maafisa wa kifalme wamekuja ili
kumtakia heri bwana wetu mfalme Daudi
wakisema, ‘Mungu wako na alifanye jina la
Solomoni kuwa mashuhuri kuliko lako na kiti
chake cha ufalme kiwe na ukuu kuliko chako!’
Naye mfalme akasujudu akiabudu kitandani
mwake 48 na kusema, ‘Ahimidiwe BWANA wa
Israeli, ambaye ameruhusu macho yangu kuona
mrithi juu ya kiti changu cha ufalme leo hii.’ ’’
49 Katika hili, wageni wote wa Adonia
wakainuka kwa mshtuko wa hofu na
kutawanyika. 50 Lakini Adonia kwa kumwogopa
Solomoni, akaenda na kushika pembe za
madhabahu. 51 Kisha Solomoni akaambiwa,
“Adonia anamwogopa Mfalme Solomoni na
ameshikilia pembe za madhahabu. Anasema,
‘Mfalme Solomoni na aniapie leo kwamba
hatamwua mtumishi wake kwa upanga.’ ’’
52 Solomoni akajibu, “Kama akijionyesha
kuwa mtu mstahiki, hakuna unywele wake
utakaoanguka juu ya ardhi, lakini kama uovu
ukionekana ndani yake, atakufa.’’ 53 Ndipo
Mfalme Solomoni akawatuma watu, nao
wakamshusha kutoka madhabahuni. Naye
Adonia akaja akamwinamia Mfalme Solomoni,
naye Solomoni akamwambia, “Nenda nyumbani
kwako.’’
Maa
gizo Ya Daudi Kwa Solomoni
2
Siku zilipokaribia za Daudi kufa, akampa
mwanawe Solomoni agizo,
2 akasema, “Mimi ninakaribia kwenda njia ya
dunia yote. Hivyo uwe hodari, jionyeshe kuwa
mwanaume, 3 shika lile BWANA wako
analokuagiza: Enenda katika njia zake, ushike
maagizo na amri zake, sheria zake na kanuni
zake, kama ilivyoandikwa katika Sheria ya
Mose, ili upate kustawi katika yote ufanyayo na
po pote uendako, 4 ili kwamba BWANA aweze
kunitimizia ahadi yake: ‘Kama wazao wako
wakiangalia sana wanavyoishi na kama
wakienenda kwa uaminifu mbele zangu kwa
3
952102164.004.png
 
1 WAFALME
mioyo yao yote na kwa roho zao zote, kamwe
hutakosa kuwa na mtu kwenye kiti cha ufalme
cha Israeli.’
5 “Sasa wewe mwenyewe unafahamu lile
Yoabu mwana wa Seruya alilonitendea, lile
alilofanya kwa majemadari wawili wa majeshi ya
Israeli, Abneri mwana wa Neri na Amasa mwana
Yetheri. Aliwaua, akimwaga damu yao wakati wa
amani kama vile ni kwenye vita, tena akaipaka
damu ile kwenye mkanda uliokuwa kiunoni
mwake na viatu alivyovaa miguuni mwake.
6 Shughulika naye kwa kadiri ya hekima yako,
lakini usiache kichwa chake chenye mvi kishukie
kaburi a kwa amani.
7 “Lakini uwaonyeshe wema wana wa
Barzilai wa Gileadi na uwaruhusu wawe
miongoni mwa wale walao mezani pako.
Walisimama nami nilipomkimbia ndugu yako
Absalomu.
8 “Ukumbuke, unaye Shimei mwana wa
Gera, Mbenyamini, kutoka Bahurimu, ambaye
alinilaani kwa laana kali siku niliyokwenda
Mahanaimu. Aliposhuka kunilaki huko Yordani,
nilimwapia kwa BWANA : ‘Sitakuua kwa
upanga!’ 9 Lakini sasa, usidhani kwamba hana
hatia. Wewe ni mtu wa hekima, utajua la
kumtendea. Zishushe mvi zake kaburini kwa
damu.’’
10 “Kisha Daudi akapumzika pamoja na baba
zake naye akazikwa katika Mji wa Daudi.
11 Alikuwa ametawala juu ya Israeli miaka
arobaini, miaka saba huko Hebroni na miaka
thelathini na mitatu katika Yerusalemu. 12 Kwa
hiyo Solomoni akaketi katika kiti cha ufalme cha
baba yake Daudi, nao utawala wake ukaimarika
sana.
17 Kwa hiyo akaendelea kusema, “Tafadhali
mwombe mfalme Solomoni, anipatie Abishagi
Mshunami awe mke wangu, hatakukatalia
wewe.’’
18 Bathsheba
akamjibu,
“Vema
sana,
nitazungumza na mfalme kwa ajili yako.’’
19 Bathsheba alipokwenda kwa Mfalme
Solomoni kuzungumza naye kwa ajili ya Adonia,
mfalme alisimama kumlaki mama yake,
akamwinamia na kuketi kwenye kiti chake cha
ufalme. Akaamuru kiti cha ufalme kuletwa kwa
ajili ya mama yake mfalme, naye akaketi mkono
wake wa kuume.
20 “Bathsheba akamwambia mfalme, “Ninalo
ombi moja dogo la kukuomba, usinikatalie.’’
Mfalme akajibu, “Omba mama yangu,
sitakukatalia.’’
21 Akasema, “Mruhusu Abishagi Mshunami,
aolewe na ndugu yako Adonia.’’
22 Mfalme Solomoni akamjibu mama yake,
“Kwa nini uombe Abishagi Mshunami kwa ajili ya
Adonia? Ungeweza pia kuomba ufalme kwa ajili
yake, hata hivyo, yeye ni ndugu yangu mkubwa,
naam, pia kuhani Abiathari na Yoabu mwana wa
Seruya wapo upande wake!”
23 Mfalme Solomoni akaapa kwa BWANA,
akasema: “Mungu na aniulie mbali, tena bila
huruma, ikiwa Adonia hatalipa kwa uhai wake
kwa ajili ya ombi hili! 24 Basi sasa, hakika kama
BWANA aishivyo, yeye ambaye ameniimarisha
salama kwenye kiti cha ufalme cha Daudi baba
yangu naye amenipatia ukoo wa kifalme kama
alivyoahidi, Adonia atauawa leo!’’ 25 Hivyo
mfalme Solomoni akatoa amri kwa Benaya
mwana wa Yehoyada, naye akampiga Adonia
akafa.
26 Mfalme akamwambia kuhani Abiathari,
“Nenda huko Anathothi katika mashamba yako.
Wewe unastahili kufa, lakini sitakuua sasa, kwa
sababu ulilichukua sanduku la BWANA
Mwenyezi mbele ya Daudi baba yangu na
ulishiriki taabu zote za baba yangu.’’ 27 Hivyo
Solomoni akamwondoa Abiathari kwenye
ukuhani wa BWANA, akilitimiza neno la BWANA
alilokuwa amenena huko Shilo kuhusu nyumba
ya Eli.
28 Habari zilipomfikia Yoabu, ambaye alikuwa
amefanya shauri baya na Adonia, Absalomu
hakuhusika, alikimbilia kwenye hema la BWANA
na kushika pembe za madhabahu. 29 Mfalme
Solomoni akaambiwa kuwa Yoabu amekimbilia
kwenye hema la BWANA naye alikuwa kando ya
madhabahu. Basi Solomoni akamwagiza
Kiti Cha Ufalme Cha Solomoni Chaimarishwa
13 Basi Adonia, mwana wa Hagithi, akaenda
kwa Bathsheba, mama yake Solomoni.
Bathsheba akamwuliza, “Je, umekuja kwa
amani?’’ Akajibu, “Ndiyo, kwa amani.” 14 Kisha
akaongeza, ‘‘Ninalo jambo la kukuambia.’’
Akajibu, “Waweza kulisema.’’
15 Akasema, “Kama unavyojua, ufalme
ulikuwa wangu. Israeli wote waliniangalia mimi
kama mfalme wao. Lakini mambo yalibadilika,
ufalme umekwenda kwa ndugu yangu, kwa
maana umemjia kutoka kwa BWANA. 16 Sasa
ninalo ombi moja ninalokuomba. Usinikatalie.’’
Bathsheba akasema, “Waweza kuliomba.’’
a 6 “Kaburi” maana yake hapa ni “Kuzimu,” yaani, Sheol kwa
Kiebrania.
4
952102164.001.png
 
1 WAFALME
Benaya
mwana
wa
Yehoyada:
“Nenda
na kukuonya kuwa, ‘Siku utakayoondoka
kwenda mahali pengine po pote, uwe na hakika
utakufa?’ Wakati ule uliniambia, ‘Ulilolisema ni
jema. Nitatii! 43 Kwa nini basi hukutunza kiapo
chako kwa BWANA na kutii amri niliyokupa?’’
44 Pia mfalme akamwambia Shimei, ‘‘Unajua
katika moyo wako, makosa uliyomtendea baba
yangu Daudi. Sasa BWANA atakulipiza kwa ajili
ya mabaya yako uliyotenda. 45 Lakini mfalme
Solomoni atabarikiwa, na kiti cha ufalme cha
Daudi kitakuwa imara mbele za BWANA milele.’’
46 Kisha mfalme akatoa amri kwa Benaya
mwana wa Yehoyada, naye akatoka nje
akampiga Shimei na kumwua.
Sasa ufalme ukawa umeimarika kikamilifu
mikononi mwa Solomoni.
ukamwue!’’
30 Ndipo Benaya akaingia kwenye hema la
BWANA na kumwambia Yoabu, “Mfalme
anasema, ‘Toka nje!’ ’’
Lakini akajibu, “La! Nitafia hapa hapa.’’
Benaya akamwarifu mfalme, “Hivi ndivyo
Yoabu alivyonijibu.
31 Kisha mfalme akamwamuru Benaya,
“Fanya kama asemavyo. Mwue na kumzika, ili
uniondolee mimi na nyumba ya baba yangu
dhambi ya damu isiyokuwa na hatia ile Yoabu
aliyoimwaga. 32 BWANA atamlipiza kwa ajili ya
damu aliyoimwaga, kwa sababu, pasipo Daudi
baba yangu kujua, aliwashambulia watu wawili
na kuwaua kwa upanga. Wote wawili, Abneri
mwana wa Neri, jemadari wa jeshi la Israeli na
Amasa mwana wa Yetheri, jemadari wa jeshi la
Yuda, ambao walikuwa watu wazuri na wanyofu
kuliko yeye. 33 Hatia ya damu yao na iwe juu ya
kichwa cha Yoabu na wazao wake milele. Lakini
kwa Daudi na uzao wake, nyumba yake na kiti
chake cha ufalme, iwepo amani ya BWANA
milele.’’
34 Basi Benaya mwana wa Yehoyada
akakwea, akampiga na kumwua Yoabu, naye
akazikwa katika nchi yake mwenyewe katika
jangwa. 35 Mfalme akamweka Benaya mwana wa
Yehoyada juu ya jeshi kwenye nafasi ya Yoabu
na kumweka kuhani Sadoki badala ya Abiathari.
36 Kisha mfalme akatuma ujumbe kwa
Shimei na kumwambia, “Ujijengee nyumba huko
Yerusalemu uishi huko, lakini usiende mahali
pengine po pote. 37 Siku utakayoondoka kuvuka
Bonde la Kidroni, uwe na hakika utakufa, damu
yako itakuwa juu ya kichwa chako mwenyewe.’’
38 Shimei akamjibu mfalme, “Ulilolisema ni
jema. Mtumishi wako atatenda kama bwana
wangu mfalme alivyosema.’’ Naye Shimei
akakaa Yerusalemu kwa muda mrefu.
39 Lakini baada ya miaka mitatu, watumwa
wawili wa Shimei wakatoroka kwenda kwa
Akishi mwana wa Maaka, mfalme wa Gathi,
naye Shimei akaambiwa, “Watumwa wako wako
Gathi.’’ 40 Kwa ajili ya hili, Shimei akatandika
punda wake, akaenda kwa Akishi huko Gathi
kuwatafuta watumwa wake. Basi Shimei
akaondoka na kuwarudisha watumwa wake
kutoka Gathi.
41 Solomoni alipoambiwa kuwa Shimei
ametoka Yerusalamu na kwenda Gathi na
amekwisha kurudi, 42 mfalme akamwita Shimei
na kumwambia, “Je, sikukuapiza kwa BWANA
Solomoni Anaomba Hekima
Solomoni akafanya urafiki na Mfalme
Farao wa Misri na kumwoa binti yake.
Akamleta huyo binti katika mji wa Daudi mpaka
alipomaliza kujenga jumba lake la kifalme na
hekalu la BWANA, pamoja na ukuta kuzunguka
Yerusalemu. 2 Hata hivyo, watu bado walikuwa
wakitoa dhabihu huko kwenye vilima, kwa
sababu hekalu lilikuwa bado halijajengwa kwa
ajili ya Jina la BWANA. 3 Solomoni akaonyesha
upendo wake kwa BWANA kwa kuenenda
sawasawa na amri za Daudi baba yake, ila yeye
alitoa dhabihu na kufukiza uvumba huko mahali
pa juu.
4 Mfalme akaenda Gibeoni kutoa dhabihu,
kwa maana ndipo palipokuwa mahali maarufu
zaidi, naye Solomoni akatoa sadaka elfu moja
za kuteketezwa juu ya hiyo madhabahu.
5 BWANA akamtokea Solomoni huko Gibeoni
wakati wa usiku katika ndoto, naye Mungu
akasema, ‘‘Omba lo lote utakalo nikupe.’’
6 Solomoni akajibu, ‘‘Umemfanyia mtumishi
wako baba yangu Daudi fadhili nyingi, kwa kuwa
alikuwa mwaminifu kwako na mwenye haki tena
mnyofu wa moyo. Nawe umemzidishia fadhili hii
kuu na umempa mwana wa kuketi kwenye kiti
chake cha ufalme kama ilivyo leo.
7 Sasa, Ee BWANA wangu, umemfanya
mtumishi wako mfalme baada ya baba yangu
Daudi. Lakini mimi ni mtoto mdogo tu wala sijui
jinsi ya kutekeleza wajibu wangu. 8 Mtumishi
wako yuko hapa miongoni mwa watu
uliowachagua. Taifa kubwa, watu wengi
wasioweza kuhesabika wala kutoa idadi yao.
9 Hivyo mpe mtumishi wako moyo wa ufahamu
kutawala watu wako na kupambanua kati ya
3
5
952102164.002.png
 
Zgłoś jeśli naruszono regulamin